MEYA WA JIJI LA TANGA MHINA MUSTAFA SELEBOS AKIZUNGUMZA WAKATI WA HAFLA YA UZINDUZI WACHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI WA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 14 MKOANI TANGA.
Hassan Hashim Tanga.
Waziri wa Afya maendeleo ya jami jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amewataka wakuu
wa Mikoa na Halmashauri kutenga siku
moja kila mwezi kwa ajili ya
kutoa huduma za upimaji wa saratani za aina mbalimbali ikiwemo tezi dume .
Kauli hiyoa ameitoa wakati akizindua utoaji wa chanjo
ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa chini ya miaka 15
mkoani Tanga.
Amesema upimaji wa saratani ndio njia pekee
itakayowezesha wananchi kujitambua mapema
ambapo watakaogundulika katika hatua za
awali wanaweze kupatiwa matibabu na kupona.
Aidha Waziri Ummy amewataka watumishi wa afya
kutotoa chanjo kwa watoto ambao wazazi
wao au walezi hawajaridhia
.
Awali
akizungunza katika uzinduzi huo kaimu Mkuu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga
Dkt Clemence Marcel amesema mkoa wa tanga unatarajia kutoa chanjo kwa wasichana
38,000 wakiweomo wanafunzi na makundi mengine.
…………………….
|
No comments: