ZOEZI LA UHAKIKI WA MIFUGO LAPATA MUITIKIO MKUBWA WILAYA YA HANDENI
Add caption |
Wafugaji wilayani Handeni mkoani
Tanga wametakiwa kuitikia kwa vitendo agizo la serikali kwa kufikisha mifugo
yao katika maeneo husika ili ihakikiwe na kuwekewa alama za utambuzi
Agizo hilo limetolewa na
mkuu wa wilaya ya Handen Godwin Gondwe katika hafla ya uzinduzi wa upigaji
chapa mifugo iliyofanyika katika kijiji
cha Sua wilayani humo.
Amesema lengo la serikali
la kuweka alama za mifugo ni kuwezesha kutambua mifugo iliyopo katika maeneo
mbalimbali na kudhibiti uingizaji wa mifugo kiholela kutoka maeneo mengine
ambayo imekuwa chanzo cha migogoro kati
ya wakulima na wafugaji .
Kwa upande wao baadhi ya
wafugaji wamepongeza zoezi hilo na kuiomba serikali kuharakisha mpango wa
matumizi bora ya ardhi ambao utaanisha maeneo ya malisho ili kuondoa migogogo.
Zaidi ya ng’ombe 1,31,000 Wilaya
ya Handeni wanatarajiwa kupigwa chapa
ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali la kuhakiki na kutambua mifugo yote iliyopo
nchini.
…………………………….
No comments: