TAASISI ZA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI ZATAKIWA KUWEKA MKAKATI ILI KUFIKIA MALENGO
WAZIRI WA MAJI ISSACK KAMWELE AKIHUTUBIA VIONGOZI WA TAASISI ZA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI. |
WAZIRI WA MAJI ISSACK KAMWELE AKIKAGUA MITAMBO YA KUTIBU MAJI TANGA UWASA. |
WAZIRI WA MAJI ISSACK KAMWELE AKITEMBELEA KUKAGUA VYANZO VYA MAJI TANGA UWASA |
|
Hassan Hashim Tanga .
Taasisi na Mamlaka za
maji nchini zimetakiwa kuweka mkakati
utakaofanikisha kufikia malengo ya serkali upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 75
% ifikapo juni mwaka 2018.
Agizo hilo limetolewa na
waziri wa maji mhandisi Issack Kamwele
wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mamlaka za maji nchini unaofanyika jijini
hapa.
Amesema uzoefu uliopatkana katika mamlaka za maji
mijini kuongeza upatikanaji wa huduma ufikishwe katika ngazi za halmashuari ili
kufikia malengo la serikali ya kuboresha huduma za maji kwawananchi wote .
Amesema tangu kuanzishwa
kwa program ya maendelo ya maji serikali imelenga kuanzisha vituo vya
kutolea maji 117,000 lakini kutokana na uharibifu wa mazingir asilimia
35 havitoi maji .
Awali akimkaribisha
waziri mwenyekiti ATAWAS Mkama Bwire amesema
Changamoto iliyopo kwa hivi
sasa niupatikanaji wa rasilimali ya uendelezaji wa miradi ya utoaji wa huduma za maji
Mkutano huo unashirikisha
wadau wa sekta ya maji zikiwemo mamlaka vyuo watafiti na watoji wa huduma
mbalimbali.
No comments: